Na . Yuster Sengo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ulanga ndugu, Jonas Mallosa amewataka madiwani kuwa wajibisha watumishi wasiowajibika katika majukumu yao ili kurejesha nidhamu ya kazi katika halmashauri .
Akizungumza katika kikao cha baraza la taarifa cha halmashauri ya wilaya ya ulanga, Mallosa amesema kuwa ni vyema madiwani kuwashauri watumishi pamoja watendaji wa vijiji kuwajibika katika kazi na kuwatahadhalisha watumishi wote wasio wajibika kuondolewa kazini.
“Waheshimiwa tuache tabia ya kuwakingia kifua watumishi wazembe na badala yake tuwashauri kufanya kazi kwa weledi na kujituma kwa ustawi wa halmashauri yetu”amesema Mallosa
Aidha amewataka madiwani kuwasimamia pasipo kuogopa lawama hali inayopelekea kuvunjika kwa miiko ya utumishi wa uma na kujikuta wakikubaliana na mambo yanayoweza kuharibu utaratibu wa kazi.
“Kwenye utendaji lawama haziwezi kuepukika, tusiogope lawama kama kile kinachofanyika kiko sahihi kwa mujibu wa sheria na utaratibu,hivyo niwasihi madiwani tuwalee hawa watumishi lakini wanapo enda tofauti tuwaonye pia “ameongeza mallosa
Hatahivyo ametoa rai kwa madiwani hao kuondoka katika mambo yanayoweza kuathiri utendaji wao wa kazi kwa badala yake kufanyakazi kwa kufuata sheria na utaratibu unaotakiwa.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.