ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Mbunge wa jimbo la Ulanga mh Goodluck Mlinga amezindua kiwanda cha chaki na sabuni kilichopo kata ya Mahenge Mjini Wilayani Ulanga huku akiwataka wanachi kuonyesha uzalenda kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika tarehe 4/8/2018 Mh Mlinga amesema kuwa kiwanda hicho kimetoa ajira kwa wazawa na kukuza uchumi wa familia zao hivyo amewataka wafanyakazi wazawa waliopata fursa ya kazi katika kiwanda hicho kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kukiwezesha kiwanda kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha Mh Mlinga amewataka wananchi wengine na hasa wazawa wenye uwezo wa kuanzisha viwanda mbalimbali wafanye hivyo ili kutoa fursa ya ajira zaidi kwa wazawa na maendeleo ya jimbo la ulanga kwa ujumla kwani itasaidia kuajiri vijana wengi na pia kuendana na dhana ya Nchi ya Viwanda,kuboresha uchumi na kuleta maendeleo endelevu kwa kufikia uchumi wa kati.
Kama kuna watu wana uwezo wa kujenga viwanda mbalimbali tunaomba mfanye hivyo vijana wetu waweze kupata ajira ili waweze kujikwamua kimaisha na kuepukana na tabia mbaya ikiwemo kukaa vijiweni,kuvuta bangi na kufanya biashara haramu.
Kiwanda hicho kina mashine tatu ndogo za mkononi ambazo hazitumii umeme na zimegharimu shilingi milioni thelathini na tano na pia imeznza kusambaza bidhaa zake katika shule mbalimbali ikwemo za msingi na sekondari na imeajiri wafanyakazi kumi wakiwemo wanawake watano na wanaume watano na kinasaidia shughuli za kijamii kama vile Printer na Computer .
Hata hivyo kiwanda hicho kinatekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi kama kinavyosema kuwa Tanzania ya Viwanda na hata kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh.dk.John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.