ULANGA
NA Fatuma Mtemangani
Afisa mazingira wilayani ulanga bwana Jastin Bundu amewapongeza Wananchi wilayani ulanga mkoani morogoro kwa kuimarisha usafi wa mazingira katika maeneo yao hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika na kuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza.
Aidha bwana Bundu amewata wale wote ambao vyoo vyao vimeharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha wanarekebisha vyoo hivyo ama kujenga upya ili kulinda afya za watumiaji.
Hata hivyo amewatahadharisha baadhi ya wananchi wenye tabia ya tabia ya kutiririsha maji machafu kwenye mifereji waache mara moja hivyo wanapaswa kufanya usafi kwa kufyeka majani kwenye makazi yao ili kuepukana na magonjwa hatari ikwemo ugonjwa wa homa ya matumbo,kipindupindu na malaria.
“Nasema kuanzia leo tutafuata sheria za mazingira kama zinavyoelekeza kwa yeyote atakaekiuka kuimarisha usafi wa mazingira katika eneo lake atatozwa faini ya shilingi elfu hamsini papo hapo Ili kuepukana na magonjwa yasiyo lazima,hivyo kila mwananchi anapaswa kuwa na choo bora na kuhifadhi taka kwenye mifuko na kuzipeleka kwenye kizimba kilicho karibu yake.alisema Bundu.
Bwana Bundu ameongeza kuwa serikali ina mtandao mkubwa wa kutoa elimu kwa wananchi kwani wana wawakilishi kuanzia ngazi za vijiji kata tarafa hadi wilaya hivyo wananchi mnatakiwa kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa mazingira.
sambamba na hilo ameitaka jamii kutobweteka kutokana na wilaya ya ulanga kupita salama katika kipindi cha masika kwa mwaka uliopita na hata mwaka huu hakuna mlipuko wowote uliojitokeza mpaka sasa hivyo jamii inatakiwa kuishi kwa kufuata sheria na kanuni bora za mazingira.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.