Waheshimiwa madiwani wa wilaya ya ulanga mkoani morogoro wamependeeza kutumia shilingi milioni kumi kwaajili ya kuchimba visima katika kata ya ruaha na chilombora kutokana na ukosefu wa maji safi na salama
Hatua hiyo imekuja baada ya madiwani wa kata hizo mbili kuwasilisha taarifa iliyoonyesha changamoto ya maji hali inayopelekea wakazi wa kata hizo kupata maji yenye tope ambayo si safi na salama.
Akizungumza katika kikao hicho cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ulanga mh.furaha lilongeli amewaomba madiwani kukubaliana kwa pomoja kutumia pesa hizo ili kutatua changamoto zilizopo katika kata hizo.
Wananchi wa kata za chilombora na ruaha wanateseka kutokana na kukosa maji safi na salama na wakati mwingine inawalazimu kunywa maji yasiyo faa kwa afya ya binadamu
Mwa upande wake muhandisi wa maji wilaya ya ulanga bw. david kaijage amesma kuwa hadi sasa wameshindwa kumaliza tatizo hilo kutokana na pesa walizoomba kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya maji bado hazijafika ofisini kwake.
Miundo mbinu ya maji katika kata ya ruaha na chilombora iliharibiwa vibaya kutokana na mvua zilizo nyesha mwezi wanne mwaka 2017 na kusababisha wakazi hao kupata adha kubwa ya maji hali ambayo inawea kupelekea adhari kubwa za kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.