Wananchi wilayani ulanga mkoani morogoro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye wiki ya sheria ili kufahamu mambo mbalimbali yanayohusiana na sheria.
Hayo yamesemwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya ulanga mh. James mhanus wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria kwa wilaya ya ulanga na kuongeza kuwa elimu hiyo inafaida kubwa kwa jamii kwa kuwa watajifunza mambo mbalimbali yanayaotolewa na wadau mbalimbali wa mahakama kama vile ustawi wa jamii, takukuru, polisi, magereza na mahakama zenyewe.
“nawaomba wakazi wa wilaya hii wajitahidi kujitokeza na kuhudhuria wiki ya sheria ili kuweza kujifunza mambo mbali mbali hususani mambo ya sheria na pia watajifunza mambo mbali mbali kutoka takukuru,polisi,magereza,na mahakamani pi”Amesema Mhanus
Uzinduzi huo umefanyika leo 25/1/2021 katika gereza la mahenge ambapo wafungwa pomoja na mahabusu wamepata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na changamoto wanazokutana nazo na kwa upande wa mahakama na mwendesha mashtaka amejibu na kutatua baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa ndani ya uwezo wao.
Hata hivyo mahabusu wametoa shukrani zao kwa mahakama na muendesha mashtaka kwa kuwa wamewajali na kuwathamini kwa kuweza kufanya uzinduzi huo katika gereza la mahenge.
Aidha mh. Hakimu pamoja na muendesha mashtaka wa jeshi la polisi inspekta simon mgonja, wametoa wito kwa wafungwa watakao maliza muda wao na mahabusu ambao watakaokuwa hawana hatia waende wakawe raia wema kwenye jamii na sio kurudia makosa.
Wale ambao wata,maliza muda wao humu ndani ,tunawashauri wakawe raia wema huko waendako na waepuke kurudia makosa ambayo yatawafanya kurudishwa humu ndani .”Amesema Muhanus
Wiki ya sheria itaendelea hadi tarehe 29/1/2021 ambapo kwa siku ya kesho 26/1/2021 mahakama itaendelea kutoa elimu katika shule sekondari nawenge
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.