KATIBU TAWALA WA MKOA WA MOROGORO ENG NDUGULU AMEWATAKA MAAFISA TEHAMA NA MAAFISA HABARI KUWACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI KWA WELEDI ILI KUTOA TAARIFA NA MATUKIO YANAYOTOKEA NDANI YA HALMASHAURI ZAO.
ENG.NDUNGULU AMEYASEMA HAYO KWENYE UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MAAFISA HABARI NA TEHAMA YANAYOENDELEA KATIKA UKUMBI WA EDEMA HOTEL MKOANI MOROGORO KWA LENGO LA KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA TAARIFA MBALIMBALI.
HATA HIVYO AMESEMA KUA HII NI HAKI YAO KUPATA TAARIFA YA MATUKIO YOTE YANAYOTOKEA DUNIANI HIYVO ZITASAIDIA KUWAPATIA HUDUMA BORA WANANCHI ILI KUONDOA UMASKINI KWA KUWAPATIA HABARI KWA WAKATI.
KWA UPANDE WA WASHIRIKI HAO WAMESEMA KUA CHANGAMOTO KUBWA NI UCHELEWASHWAJI WA TOVUTI KATIKA HALMASHAURI PAMOJA NA TATIZO LA MTANDAO JAMBO AMBALO LINAWAPELEKEA KUTO FANYA KAZI KWA WAKATI.
MAFUNZO HAYO YA MAAFISA TEHAMA NA MAAFISA HABARI WAPATAO 86 KUTOKA MIKOA MBALIMBALI WAMEPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA TOVUTI MKOANI MOROGORO.
MAFUNZO HAYO YAMEFANYIKA KATIKA UKUMBI WA EDEMA MKOANI MOROGORO YAKIJUMUISHA MIKOA MITANO IKIWEMO MKOA WA KILIMANJARO,ARUSHA,TANGA ,SIMIYU PAMOJA NA MOROGORO.
MGENI RASMI KATIKA MAFUNZO HAYA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA MOROGORO BWANA ENG.NDUNGURU NA AMEWASHUKURU WAFADHILI WA MRADI HUO WA TOVUTI KWA KUANDAA MAFUNZO HAYO KWA KUSHIRIKIANA NA OFISI YA TAMISEMI.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.