Ulanga
na Fatuma Mtemangani
Redio ulanga imefanya vizuri kipindi cha kilimo kwanza kwa mwaka 2017 kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima kupitia sekta ya kilimo kutokana na vipindi vinavyo fanywa kila siku ya alhamisi kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la ANSAF.
Hii imesaidia kwa wakulima kwanza kujua kilimo cha kisasa na chenye tija,kuwapatia wakulima jukwaa la kuelezea changamoto zinazowakabili kupitia redio Ulanga hasa katika zao la mpunga,namna ya kuandaa shamba, mbegu bora za kupanda shambani,muda wa kupanda mbegu shambani,muda wa kupalilia mazao pamoja na kuvuna.
Hata hivyo kuwawezesha wakulima kupata ushauri wa kitaalam kwa kuwaunganisha na wataalamu,kuwawezesha wakulima kupaza sauti zao katika mipango na maandalizi ya sera mbalimbali na kupata fursa za masoko.
Changamoto kubwa au naweza kuliita sugu hii ni kwa tanzania nzima ni wakulima kutopata pembejeo za kilimo kwa wakati na hasa wazabuni wanao watumia wamekuwa na tabia ya kuwasinisha wakulima pembejeo ambazo sio idadi ya pembejeo waliochukua.
Aidha wananchi wamepata elimu na kuondoa uoga na kwa sasa wanahudhuria vikao vya halamashauri ya kijiji kwa kuchangia maendeleo ya kijiji husika,na wanauwezo wa kuhoji juu ya maendeleo ya halmashauri.
Pia kwa kupitia kipindi cha kilimo kwanza wakulima wa wilaya ya ulanga kwa sasa wameanza kubadilika kwani wananchi wameachana na kilimo cha mazoea na sasa wanalima kilimo cha kisasa na chenye tija,na wanalima kilimo cha umwagiliaji.
ANSAF kwa kupaza sauti zao imesaidia pia kwa ulanga kwa mwaka huu 2017 hakuna changa moto kwa wakulima kuhusu vipimo vilivyokua vikitumika kuwanyonya wakulima wakati wa mavuno kwa kuongea na afisa biashara nae kulikemea hilo,kuondoa madalali wababaishaji kwa wakulima kwa kuwabadilishia bei ya mpunga na mchele.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.