ULANGA
Na Fatuma Mtemangani
Jumla ya kaya 14,071 zenye wanachama 71,293 zimejiunga na zimeingizwa kwenye mfumo (IMIS) kwa kipindi cha Machi 2016 March 2018, sawa na asilimia 45.47 ya kaya zote za Wilaya ya Ulanga.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa bi Sigilinda Mdemu wakati akizungumza na Ulanga Fm ofisini kwake juu ya mafanikio waliyoyapata kwenye uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na bima ya chf iliyoboreshwa kwawilaya ya ulanga.
Bi Sigilinda ameongeza wananchi wa wilaya ya ulanga wamejitokeza kwa wingi kujiunga na huduma hiyo na hasa jamii ya wafugaji ambao wamekua mstari wa mbele kujiunga na huduma hiyo kwa kuwaptia elimu juu ya faida zinazopatikana na CHF iliyoboreshwa.
“Sisi timu ya CHF iliyoboreshwa tumefanya kazi kubwa sana kutoa elimu kwa jamii juu ya kujiunga na huduma hiyo hasa jamii ya wafugaji ambayo ilkua ni changamoto kubwa kutokana na uelewa mdogo waliokuwa nao lakini tunashukuru wafugaji wengi wamejitokeza na kujiunga na bima yaafya ya CHF iliyoboreshwa”.
“Pia tumetoa elimu kwa Wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa kata zote za Wilaya ya Ulanga namna ya kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF iliyoboreshwa hivyo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuifikisha elimu hii kwa jamii na mafanikio yake tunayao na tumekuwa na wanachama wengi katika huduma hiyo”.
Hata hivyo CHF iliyoboreshwa imefanikiwa Kufungua dirisha maalum kwa wanchama wa CHF kwenye vituo vya kutolea huduma,pia Kutumia Redio Ulanga Fm 91.5kutoa elimu ya CHF iyoboreshwa kwa jamii,Kuwatumia walimu kusaidia kuingiza data za wanachama wa CHF kwenye IMIS wakati wa likizo.
Pia imefanikiwa Kufanya mikutano ya uhamasishaji kwa vijiji 59 vya Wilaya ya Ulanga kwa kuwa tumia viongozi maarufu.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.