WANANCHI WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO WAMETAKIWA KUFUATILI NA KUZINGATIA TAARIFA ZINAZOTOLEWA NA MAMLAKA YA UTABIRI WA HALI YA HEWA NCHINI ILI KUEPUKANA NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA.
AKIZUNGUMZA NA ULANGA FM OFISINI KWAKE MSIMIZI WA KITENGO UTABIRI WA HALI YA HEWA MAHENGE BWANA RAMADHAN OMARI AMESEMA KUWA UTABIRI WA HALI YA HEWA NI JAMBO LINALOBADIRIKA BADIRIKA KULINGANA NA WAKATI NA HIVYO SI VEMA KWA WANANCHI KUONA WANADANGANYWA BALI WAWE NA TABIA YA KUFUATILIA HALI YA HEWA MARA KWA MARA ILI KUPATA USAHIHI ZAIDI.
AIDHA BWANA RAMADHANI AMETOA WITO KWA WANANCHI WOTE HUSUSANI WAKULIMA KUZITUMIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO ILI KUEPUKANA NA TATIZO LA NJAA LINALOWEZA KUJITOKEZA.
KULINGANA NA MAMLAKA YA UTABIRI WA HALI YA HEWA NCHINI MVUA ZINATARAJIWA KUFIKIA MWISHO KATI YA WIKI YA NNE YA MWEZI APRILI NA MWANZONI MWA MWEZI MAY MWAKA HUU.
MWISHO.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.