Ulanga
Katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro itapanda miti katika maeneo mbalimbali.
Zoezi hilo litafanyika tarafa ya vigoi katika maeneo ya Udeko,kwiro,nawenge pamoja na eneo la Hospital ya wilaya.
Pia wananchi wote pamoja na taasisi mbalimbali wametakiwa kupanda miti katika maeneo yao siku hiyo, ili kuyalinda mazingira wilayani humo.
Katika kuelekea siku ya muungano zoezi la kupanda miti litaongozwa na mkuu wa wilaya ya ulanga ndugu Joseph Jacob Kassema,Mkurugenzi mtendaji ndugu Yusuph Semuguruka,pamoja na waheshimiwa madiwani wa kata zote wilayani ulanga.
Ikumbukwe kila ifikapo tarehe 26/4 ya kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar hivyo wananchi wanapaswa kuienzi siku hiyo hivyo waheshimiwa madiwani,maafisa wa kata na vijiji wanatakiwa kusimamia zoezi hilo.
Na Fatuma Mtemangani.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.