19/01/2017 SAA 3:OOUSIKU MADINI YA KINYWE
WAKAZI WA KIJIJI CHA EPANKO WALIO KATIKA ENEO LA MRADI WA UCHIMBAJI WA MADINI YA KINYWE WAMETAKIWA KUTUMIA SIKU SITINI WALIZOPEWA YA UTHAMINI WA MARA YA PILI KABLA YA ZOEZI HILO KUKAMILIKA MAPEMA MWEZI FEBRUARI.
HAYO YAMESEMWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA WILAYA BWANA STEPHEN PUNDILE WAKATI WA KIKAO CHA KIKOSI KAZI KILICHAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA TRC MAHENGE.
BWANA.PUNDILE AMESEMA KUWA WANANCHI HAO WANAPASWA KUJUA ZOEZI HILO LINAFANYIKA KISHERIA AMBAPO MRADI HUO HAUWEZI KUSITISHWA KWA WATU HAO KUENDELEA KUGOMA KUFANYIWA UTHAMINI KWANI MRADI HUO UPO KWA AJILI YA MANUFAA YA KIJIJI, WILAYA NA NCHI KWA UJUMLA.
AIDHA AMEISHUKURU KAMPUNI YA TANZGRAPHITE{KIBARANI} KWA KUWAONGEZEA SIKU SITINI ZA KUFANYIWA TATHMINI KAYA AMBAZO AWALI HAZIKUPITIWA NA WATHAMINI KWANI NI NAFASI YAO YA MWISHO KUPEWA NA AMBAO HAWATASHIRIKI TARATIBU ZA KISHERIA ZITAFUATWA ILI KUWAONDOA.
HATA HIVYO AMEONGEZA KUWA SERIKALI IPO KWA AJILI YA KUSIMAMIA HAKI ZA WANANCHI NA KAMPUNI ILI KUHAKIKISHA KILA MTU ANAPATA ANACHOSTAHILI NA KUACHANA NA DHANA YA KUDHANI OFISI YA MKUU WA WILAYA IPO KWA AJILI YA KAMPUNI YA KIBARANI PEKEE.
AIDHA NAYE MSEMAJI WA KAMPUNI YA KIBARAN SAUDA KILUMANGA AMESEMA KUWA KAMPUNI HIYO INA NIA NJEMA NA WANANCHI NA NDIO MAANA WAMEAMUA KUTOA NAFASI YA PILI KUFANYIWA TATHMINI KWA WALIOKOSA NAFASI HIYO AWALI NA ITAENDELEA KUFANYA JITIHADA ILI KUSHIRIKIANA PAMOJA ILI KUFANYA KAZI KWA USALAMA.
MWISHO.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.