Na.Yuster Sengo
Mweyekiti Wa halmashauri ya wilaya ya wilaya ya Ulanga mh .Edson Solly Amezitaka kamati zote zinazosimamia miradi ya ujenzi wa maabara Za Shule Za Sekondari na madarasa kwa shule Za Msingi pamoja na ujenzi wa zahanati Za Vijiji kusimamia kwa ukaribu na umakini miradi Yote kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu katika miradi hiyo
Hayo ameyesema kwa nyakati tofauti katika ziara ya kamati ya fedha ,Utawala na mipango yakukagua miradi ya maendeleo iliyopatiwa fedha Za Utekelezaji ili kuona na kujiridhisha kazi zilizofanyika kutokana na fedha zilizotolewa katika miradi husika
Aidha amezitaka kamati hizo kusimamia mafundi wanaotekeleza miradi hiyo kwani mafundi hao wapo chini ya kamati hizo
“Kamati hakikisheni mna wasimamia mafundi kwenye utekelezaji wao kwakuwa wapo chini yenu ,Namnapooona kuwa kuna shida yoyote mtupe taarifa mapema ili tuone namna ya kufanya kabla Mambo Hayajaharibika. Amesemamh.Solly
“Hata hivyo nivizuri kwa Fundi Mkuu kutumia vibarua waliopo kwenye eneo La Mradi kwani itapunguza sana malalamiko kwakuwa mara nyingi hawa vibarua huwa wanafanya kazi Za Majitolea hapa sasa nivizuri Pia Kuwapa kazi ili na wao waweze kupata fedha kidogo” Ameongeza mh. Solly
Hata hivyo Mh .Solly aliwataka madiwani kusimamia na kuhamasisha wananchi katika majitoleo ya nguvu kazi ili miradi imalizike kwa wakati na kuokoa fedha zinazoelekezwa kwenye miradi hiyo na kuanzisha majengo mengine kwa pesa zinazobaki kwenye mradi husika
“Kukiwa na nguvu kazi Za Kutosha ,Maboma yanasimamishwa kwa muda mfupi na bila gharama,Hivyo tukipata fedha Za Umaliziaji zinakuwa zinatosha kabisa na zinzazobakia tunaweza kutelekeza kwenye ujenzi wa Jengo Lingine kama ambavyo wamefanya baadhi ya maeneo tuliyopita”Amesema Mh.Solly Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga
“Na jambo linguine tuhakikishe wananchi wanaondoa siasa kwenye maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo wanazorotesha maendeleo katika vijiji vyao “Ameongeza Mh.Solly
Kwa Upande Wake Diwani wa Lukande Mh .Novatus majiji alisema kuwa jamii inapaswa kushirikishwa katika miradi Yote Inapatiwa fedha Za Utekelezaji na serikali
“Nilazima jamii zetu zishirikishwe kwenye miradi ya maendeleo ili waweze kuchangia nguvu kazi na tukumbuke kwamba nguvu kazi hizi zinasaidia sana kwenye kuokoa pesa ambazo zinaweza kutekeleza miradi mingine ndani ya eneo husika”Amesema Mh.Majiji
Akizungumza katika kikao Cha Kamati ya fedha na mipango wakati wa kujadili taarifa ya ziara ya kamati ya fedha, Utawala na mipango mwenyekiti wa halamashauri ya wilaya ya Ulanga Mh.Edson Solly Amemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga ndg.Jonas Mallosa kuliangalia kwa jicho La Pili suala la Nguvu kazi katika kata ya Mahenge kwani kumeonekana Hakuna Kabisa nguvu kazi na badala yake miradi inatekelezwa kwa kutumia fedha kuanzia mwanzo wa mradi hadi kumalizia mradi
“Nikuombe mkurugenzi lifanyie kazi suala la nguvu kazi katika eneo hili La Mahenge,kwani sehemu nyingine ukiwapa milioni thelathini wanafanya na kazi za ziada,lakini hapa wataitumia yote na muda mwingine inaweza isitoshe kwakuwa hawatumii nguvu kazi kabisa “Amesema Mh.Solly
Aidha kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga Ndg .Jonas Mallosa amesema kuwa kazi zote zinafanyika vizuri kwasababu ya ushirikiano mkubwa baina ya menejimenti na madiwania mbao wamekuwa wakisimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili iweze kuisha kwa wakati uliopangwa
“Na Pia Niwashukuru watu wasali pamoja na Gombe Kwani walikuwa nyuma sana lakini kwa sasa kutokana na ushirikiano uliokuwepo wanaendelea vizuri na inawezekana wakakamilisha kwa wakati uliopangwa “Amesema Ndg. Mallosa
Jumla ya miradi iliyokaguliwa na kamati ya fedha,Utawala na mipango ni miradi 16 Ambayo ni miradi ya umaliziaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule Za Sekondari,Umaliziaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule Za Msingi pamoja na umaliziaji wa ujenzi wa zahanati Za Vijiji ,ambapo madiwani tisa na wataalam wa halmashauri walishiriki katika ziara hiyo ya siku mbili.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.