ULANGA
NA
Fatuma Mtemangani
Kamati ya bunge ya Maliasili Utalii na Ardhi imefanya ziara wilayani Kilombero kukagua utekelezaji wa program ya mradi wa umilikishwaji wa mradi unaowezesha,kupanga na kupima ardhi unaotekelezwa katika wilaya tatu za Kilombeo,Ulanga na Malinyi
kamati hiyo imeongozwa na mwenyekiti wake mh Nape Nnauye na pia mbunge wa jimbo la Mtama imeelezea lengo la ziara hiyo ni kutaka kuona namna program hiyo ya kuwezesha umilikishaji wa ardhi kwa wananchi vijijini unavyotekelezwa katika wilaya hizo tatu kwa muda uliopangwa.
Kamati hiyo imeridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wanaotekeleza mradi huo ambapo walitembelea ofisi za kijiji cha Siginali wilayani Kilombero na kijiji cha Mbuga wilayani Ulanga ili kujiridhisha na kazi zinazofanywa na viongozi hao waliopewa dhamana ya kusimamia mradi huo ambapo wamejionea wananchi wakipokea Hatimiliki zao .
Mradi huo umesaidia sana kwa wilaya hizo tatu kwa kudhibiti migogoro ya mipaka ya kiutawala ya Ardhi kati ya kijiji na kijiji,wakulima na wafugaji,wafugaji na Hifadhi,wakulima kwa wakulima ambapo kwa sasa umeshapima mipaka ya vijiji 123.
Hata hivyo jumla ya mipaka 127 imepimwa ikiwemo wilaya ya Kilombero 65,Ulanga 40 na Malinyi 22 na kuandaa mipango ya matumizi ya Ardhi kwa wilaya tatu hivyo jumla ya mipango ya matumizi ya Ardhi ya vijiji 80 imeshatayarishwa hivyo kwa wilaya ya Kilombero ni 30,Ulanga 32 na Malinyi18.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo mh.Nape Nauye na kamati yake wamempongeza mratibu wa mradi huo bwana Machabe kwa kazi nzuri na uaminifu alioufanya kwa kutekeleza mradi huo kwa wakati katika wilaya hizo tatu kwa .
“Hongereni sana kwa kazi nzuri mnazozifanya mpaka leo hii sisi wanakamati tumeona kazi mnazozifanya kwa wananchi na leo hii wanapatiwa hati zao hii inaonyesha ni namna gani unafanya kazi kwa ya kuwatumikia wananchi pia tumeona changamoto mnazokumbana nazo najua zitakwisha tu.Alisema mh.Nape.”
Naye waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Willium Lukuvi alisema kuwa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kwa mkoa wa Morogoro kwa kupima mipaka ya vijiji 123 hivyo jumla ya mipaka 103 ya vijiji katika wilaya hizo tatu ikiwemo kilombero 42,ulanga 39,na malinyi 22 imepimwa bila gharama yoyote kutoka kwa wananchi.
Aidha mh Lukuvi ameseama kuwa wizara ya ardhi imejipanga kupata fedha kiasi cha shilingi bilion 150 kutoka Wold Bank kwa ajili ya kupima mipaka ya ardhi nchi nzima nah ii itasaidia kuondoa migogoro ya Ardhi kwa nchi nzima kwa vijiji mambavyo mradi huu unatarajia kuanza kazi katika vijiji husika.
Mradi wa urasimishaji wa Ardhi nchini ni mradi wa miaka mitatu hivyo umesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro mikubwa ya Ardhi katika wilaya ya Kilombero,Ulanga na Malinyi na wananchi wamepatiwa hati miliki zao hivyo zoezi hilo litakamilika ifikapo february mwaka huu 2019.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.