Ulanga
na Fatuma Mtemangani
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha uponera ndugu Wiliamu Kamando mwenye umri wa miaka 32 tarehe 5/12/2017 amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ulanga kwa makosa matatu tukio lililotokea tarehe 30/11/2017 saa nane kamili usiku katika kijiji cha Vigoi Juu.
Kosa la kwanza lilikuwa ni kuchomwa moto nyumba ya bwana Roki Liganga mkazi wa Vigoi Juu na kusababisha vitu mbalimbali kuungua vyenye thamani ya shilingi milioni kumi laki sita na sabini elfu.
Kosa la pili ni kumchoma moto mke wake Bi.Karista Liganga mwenye umri wa 27 ambae anakaa kwa wazazi wake na kosa la tatu ni kumchoma mtoto wake Joseph Kamando mwenye umri wa miaka miwili.
Akisomewa mashitaka hayo mbele ya hakimu mfawidhi wa Wilaya ya Ulanga Mh. Martha Mahumbuga mwendesha mashitaka inspecta wa polisi simon Mgonja ameiambia mahakama kua mshitakiwa huyo hastahili kupata dhamana.
Mtuhumiwa huyo amekosa dhamana kutoka na sababu tatu sababu ya kwanza ni kua mshitakiwa huyo akiwa nje ni hatari kwa usalama wa maisha yake kutokana na jamii haija furahishwa na kitendo alichokifanya.
Sababu ya pili ambayo imesababisha mshitakiwa huyo kukosa dhamana ni kutokana na majeruhi bado wanaendelea na matibabu katika hospital ya wilaya na hali yao bado sio nzuri pia mshitakiwa endapo atakua nje kwa dhamana ni rahisi kutoroka kutokana na tukio alilotenda.
Kutokana na sababu hizo mahakama imekubali na mshitakiwa amepelekwa mgerezani mpaka tarehe 3/1/2018 kesi hiyo itakapo tajwa tena.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.