ULANGA
Na
Fatuma Mtemangani
Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wilayani Ulanga ni miongoni mwa Idara zinazotoa huduma ya ushauri wa kitaalam,mafunzo kuhusu kilimo bora,Kilimo cha Umwagiliaji,hifadhi ya mazao,usindikikaji na ushirika kwa lengo la kuiwezesha jamii kupata tija katika uzalishaji wa mazao katika jamii.
Akizungumzia utekelezaji huo afisa mazao wilayani Ulanga bwana Revocatus Ngusa alisema kuwa idara pia inasimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji,Masoko,Maghala na kusimamia miradi ya vikundi vya uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara na Ujasiriamali katika kijiji cha Nakafulu,Idunda na Lupiro.
Hata hivyo bwana Ngusa ameongeza kuwa katika kipindi cha mwezi wa kwanza hadi wa tano Idara iliendelea kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kwa wakulima juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo cha Mazao ya Chakula ikiwemo zao la Mahindi,Mpunga,Viazi Vitamu pamoja na jamii ya Mikunde,vilevile Idara imefuatilia kwa kina Mazao ya Biashara hasa Pamba,Korosho,Kahawa na Ufuta.
“Hali ya chakula kwa Wilaya ya Ulanga ni nzuri wananchi wanapata milo miwili hadi mitatu kwa siku hii ni kutokana na baadhi ya mazao kuanza kuvunwa hasa Mahindi,Mpunga na Maharage hivyo tunaendelea kutoa ushauri kwa wakulima hao waendelee kutumia vizuri chakula walichokipata na kuacha matumizi mabaya kama vile kupika pombe za nafaka,sherehe mbalimbali na kugawa vuyakula bila mpangilio kwa watu”.
“Pia Wilaya ya ulanga ni miongoni mwa wilaya ambazo tunatekeleza ulimaji wa baadhi ya mazao mkakati matano yaliyotangazwa na serikali likiwemo zao la Pamba,Kahawa,Korosho,Chai na Katani,kati ya mazao hayo wilaya ya Ulanga tunalima zao la Pamba,Korosho na Kahawa na katika msimu wa kilimo kwa mwaka 2017/2018 wilaya imehamasisha kwa kiasi kikubwa ulimaji wa mazao haya”.
Aidha Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika imefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ununuzi wa vyombo vya usafiri kama pikipiki,mafuta ya Dizeli na Petroli kwa ajili ya maafisa ugani,Idara kwa kushirikiana na serikali kuu kusimamia upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima kwa kuchagua mawakala wenye uwezo wa kusambaza pembejeo kwa wakulima kwa wakatina kwa bei elekezi,kuendelea kuwaelimisha wakulima kupitia maafisa ugani kilimo katika maeneo walipo.
Idara pia imeendelea kutoa elimu kwa wakulima kupitia Redio Ulanga Fm juu ya kuwatambua viwavi jeshi vamizi na njia za kuwadhibiti na kuwaangamiza.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.