Na yuster Sengo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ulanga Ndg Jonas Mallosa amewaomba watumishi kuongeza nguvu kwenye vyanzo vya mapato ili kusaidia halmashauri kupata mapato ambayo yatawasaidia na watumishi katika utendaji wao
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wakati wa kikao wa kikao maalum l;a baraza la wafanyakazi cha kupokea na kujadili rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka 2021/2022
Ameongeza kuwa makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yameshuka kwa 26.16% kutoka shilingi bilion mbili milioni mia nane na sitini laki nne na thelasini na tisa kwa mwaka 2020/2021 hadi shili bilioni mbili milioni mia moja kumi na mbili na laki moja na themanini na saba kwa mwaka 2021/2022
”kiutokana na makisio hayo basi tujitahidi sana kuangalia kama kuna vyanzovipya vya kuongeza na njia bora za kukusanya mapato kwenye vyanzo tulivyonavyo “Amesa Mallosa
Akiwasilisha muhtasari wa rasimu ya bajeti kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya ulanga kaimu afisa mipango bw deogratias lihengelimo amesema kuwa baadhi ya sababu za kushuka kwa makisio ya mapato 2021/2022 ni pamoja na zaidi yab hekta elfu kumi na moja zilizokuwa zinalimwa kwenye eneo la pori tengefu la mto kilombero ambazo haztatumika tena katika uzalishaji
Ametaja sababu nyingine kuwa ni kupungua kwa idadi ya mifugo na hivyo kuathiri vyanzo vya ushuru wa minada,faini za mifugo,na mapato mengene sekta ya mifugo,sambamba na kuzuiwa kwa wavuvi kuvua katika eneo la hifadhi la mto kilombero
Aidha ameongeza kuwa sababu nyingine ni kuzuiwa kwa wavuvi kuvua katika eneo la hifadhi la mto kilombero
Hata hivyo amesema kuwa sababu nyingine ni kuondolewa kwa mapato yatokanayo na mawindo ya kitalii baada ya pori la selous kuwa hifadhi ya taifa ya nyerere
Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Ulanga imeanza mkakati wa kuongeza vyanzo vya mapato kwaajili ya kuongeza mapato kwenye halmashauri hiyo
Vyanzo vya mapato vilivyoongezwa ni pamoja na chanzo cha uogeshaji mifugo (josho)na kuanzisha msitu wa halmashauri ili kuweza kuongeza mapato kwa halmashauri
mwisho
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.