Na Alanus Matambalira
Taasisi ya kijogoo group community wilayani ulanga mkoani morogoro imefanikiwa kutoa elimu juu ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za uma katika vijiji zaidi ya 12 hadi sasa .
Katika utoaji wa elimu hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya vijiji pamoja na waratibu wa elimu ngazi ya kata ambao wote kwa pamoja wameishukuru taasis hiyo kwa elimu wanayoitoa kwa jamii kwa kuwajengea uwezo wa kuhoji mambo mbalimbali katika jamii zao
akizungumza katika mkutano wa dharura uliofanyika katika kijiji cha chikuti, msogezi , makanga , kisewe, msogezi isaka na mdindo mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Angelus Runji amesema kuwa taasis hiyo ni taasisi ya kijamiii na haifungamani wala kuwa na itikadi na siasa, ambapo pia ameongeza kuwa swala la mwananchi kufahamu mambo mbalimbali ya nayoendelea katika jamii yake ni haki yake ikiwemo taarifa ya mapato na matumizi.
Aidha Bwana Runji amefafanua kuwa toka mwaka 2017 taasisi ya kijogoo groop imekuwa ikitoa elimu hasa katika maeneo makuu matatu ndani
ya utawala bora ambapo swala la utawala bora ameitolea mfano nchi ya tanzania kuwa na misingi ya kidemokrasia huku akionya kuwa taasisi hiyo haifungamani wala kuwa na itikadi na siasa .
“tunapozungumzia swala la rasilimali za uma ni sio rasilimali ya mimi kama kiongozi sio rasilimali ya yule kama mwananchi , ni rasimali za sisi sote hiyo ndiyo rasilimali ya umma alisema mwezeshaji huyo wa mafunzo”
Hata hivyo mkurugenzi wa jkijogoo groop Bwana Ramadhani Omari amesema kuwa wao kama taasisi wanahusika kuwahamasissha wananchi na jamii kwa ujumla kufuatilia mambo malimbalimbali kwa kuhoji na kuchukua hatua juu ya rasilimali za umma.
Bw Ramadhani amezitaja rasilimali za umma kuwa ni rasilimali fedha , rasilimali watu .hivyo kwa awamu hiyo ameeleza kuwa wanaangazia hasa sekta ya elimu msingi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitolea michango mbalimbali ili kufanikisha kulisongesha mbele gurudumu la maendeleo mashuleni.
Katika mikutano hiyo wananchi pia wamepata nafasi ya kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi katika maswala ya ufuatiliaji na elimu hiyo ni endelevu katika vijiji vingine ndani ya wilaya ya ulanga
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.