Chama cha wafugaji wilayani Ulanga mkoani Morogoro kimesema uhaba wa maeneo ya malisho ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wafugaji wilayani hapa ambazo ndizo huchangia migogoro mingi ya muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji.
Chama hicho kiliyasema hayo ikiwa ni siku chache kabla viongozi wa chama hicho kutoka kila wilaya nchini kukutana na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Hassan Suluhu kujadili changamoto mbalimbali zinawakabili wafugaji nchini.
Akizungumza Mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Ulanga Bwana Peter Ndaturu alisema amefurahishwa na uamuzi wa Makamu wa Rais mama Suluhu wa kukutana na viongozi wa wafugaji huku akieleza kuwa huo ndio mwanzo wa kupata suluhu ya kudumu ya migogoro ya wakulima na wafugaji.
Aidha Bwana Ndaturu alizitaja changamoto anazotarajia kuziwasilisha kwa Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na uingizwaji holela wa mifugo katika maeneo yao, elimu duni ya ufugaji bora pamoja gharama kubwa za dawa za mifugo hali inayochangia wafugaji wa kipato cha chini kushindwa kuzimudu.
Hata hivyo katibu wa wafugaji wilayani hapa bwana Malimi Joseph amewataka wafugaji wote kuungana katika kutoa mawazo ili waweze kuyafikisha kwa serikali na baadae yakafanyiwa kazi na kuondokana na changamoto zinazo wakabili.
Mkutano wa baina ya viongozi wa wafugaji na makamu rais mama samia suluu hassan unatarajia kuanza july 11 hadi 12 mwaka huu mjini dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.