Na.Yuster Sengongo
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga limepitisha makisio ya mpango wa bajeti wa Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2023/2024 yenye jumla ya shilingi 35,218,202,000.00 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ,ruzuku ya mishahara na matumizi mengineyo
Makisio hayo yamepitishwa wakati wa mkutano wa baraza maalum la kupitisha bajeti uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa UDECO
Akiwasilisha rasimu ya makisio ya mpango wa bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Bi.Beatrice Rumbeli ambaye ni mkuu wa idara ya Mipango na Uratibu amefafanua kuwa jumla ya bajeti ni shilingi 35,218,202,000.00ambayo shilingi 3,300,000.00 ni ya mapato ya ndani ,ruzuku ya mishahara kutoka serikali kuu ni shilingi 22,892,580,000.00,ruzuku ya matumizi ya kawaida kutoka serikali kuu ni shilingi 730,304,000.00,fedha za miradi ya maendeleo ni shilingi 8,295,318,000.00
Sambamba na hilo Bi.Rumbeli amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vya Halmashauri ,baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani kwa kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato pamoja na kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ya Elimu kwa kujenga na kuboresha miundombinu
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.