Na.Yuster Sengo
BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA LEO IMEPITISHA BAJETI YA JUMLA YA SHILINGI BILIONI ISHIRINI NA SITA ,MILIONI MIA SITA ISHIRINI NA SABA LAKI NNE TISINI NA SABA ELFU NA MIA TANO (26,627,497,500) KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2010
BAJETI HIYO IMEPITISHWA KATIKA KIKAO CHA BARAZA MAALUMU LA BAJETI LILILOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PAULINE HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA NA KUJADILIWA NA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA ULANGA.
AKIWA KATIKA KIKAO HICHO MWENYEKIT WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA MH FURAHA LILONGELI AMESEMA KUWA LICHA YA KUPITISHA BAJETI HIYO AMEWATAKA WAKUU WA IDARA KUANAGALIA UWEZEKANO WA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO YA HALMASHAURI YA ULANGA
AIDHA MH LILONGELI AMESEAMA KUWA WILAYA INA VYANZO VINGI VYA MAPATO HIVYO KILA IDARA IHAKIKISHE INABORESHA VYANZO VYAKE VYA MAPATO NA KUONGEZA UWEZO WA UKUSANYAJI WA MAPATO KWANI KWA KUFANYA HIVI WILAYA ITAFIKIA MALENGO YA UKUSANYAJI WA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2010
“NAWAOMBA WAKUU WA IDARA MUWE WABINIFU WA KUVUMBUA VYANZO VYA MAPATO KATIKA IDARA ZENU ILI TUWEZE KUIONGEZEA HALMASHAURI YETU MAPATO NA HIVYO KUWEZA KUTEKELEZA KWA ASILIMIA ZOTE MIRADI YA MAENDELEO INAYO TEGEMEAMAPATO YA NDANI”AMESEMA LILONGELI
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.