• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Eneo la Utawala
    • Majukumu ya Viongozi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi na Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Radio Ulanga FM
      • Ijue Radio Ulanga FM
      • Vipindi vya Radio Ulanga FM

waziri wa mambo ya nje Palamagamba Kabudi afungua rasmi maonesho ya nane kanda ya mashariki

Imetumwa: August 2nd, 2020

Na .Yuster Sengo

Maonesho ya 27 ya wakulima nane nane yamezinduliwa rasmi leo tarehe 1/8/2020 katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika manispaa ya Morogoro

Akihutubia wakati wa zoezi la ufunguaji rasmi wa maonesho ya nane nane mwaka 2020,mgeni rasmi katika sherehe hizo waziri wa mambo ya nje  Mh Palamagamba Kabudi amesema kuwa maonesho ya mwaka huu ni ya kipekee kwasababu yanafanyika kipindi ambacho dunia imekumbwa na janga la ugonjwa wa corona lakini kwa namna ya pekee Tanzania imeweza kuhimili hali hiyo

”nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.dk John Pombe Magufuli kwa namna alivyo shughulikia jambo hili la covid-19 na hadi leo tunaendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja na kushiriki maonesho kama haya

Amesema tumefanikiwa hayo kwasababu ya uongozi madhubuti wa Mh ,Rais ,lakini pia kwa watanzania kuonesha nidhamu ya juu ya kutekeleza yale yote waliyoambiwa kuhusu tahadhari ya kupambana na ugonjwa huo

“kunawa kwa maji safi na sabuni,lakini pia kujifukiza kwa mimea mbali mbali ambayo mwenyezi mungu ameitengeneza,na leo katika maonesho haya kuna banda nimetembela na kuukuta ule mmea uliotusaidia sana kipindi cha mapambano ya corona mmea huo unaitwa kifumbasi”ameongeza Mh. Waziri Palamagamba Kabudi

Aidha ameongeza kuwa mkoa wa Morogoro umechangia sana kwa uzalishaji wa tangawizi na limao ambazo zilitumika kwa kiwango kikubwa sana wakati wa mapambano ya janga la covid -19

“niwashukuru sana wakulima wa tangawiz na limao i kwa jambo kubwa walilolifanya ,na tusilichukulie kama jambo dogo ,wakulima wa tangawizi nchini mwaka huu wametoa mchango mkubwa ambao umetunusuru na covid 19,na kikubwa hawakupandisha bei ya tangawizi wala limao

Aidha ameongeza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa watanzania kuanza kulima miti dawa au mimea dawa kwani ndani ya miaka mitano ijayo ,miti dawa na mimea dawa itakuwa ni biashara kubwa sana duniani kote

Awali akisoma taarifa ya maandalizi ya nane nane kanda ya mashariki inayo jumuiya mikoa minne ambayo ni Tanga, Morogoro ,Pwani  na Dar es salaam katibu tawala   wa Tanga amesema kuwa kwa mwaka huu wa 2020 maandalizi ya nanenane yalichelewa kuanza kutokana na sababu mbali mbali

”kwa mwaka huu maandalizi ya nane nane kanda ya mashariki yalichelewa sana kuanza kwasababu ya changamoto ya janga la  ugonjwa wa wa corona ulioukumba nchi yetu pamoja na ulimwengu kwa ujumla , lakini tunamshukuru Mungu kwa kuinusuru nchi yetu na janga hili la corona

Aidha ameongeza kuwa kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvu ,chagua viongozi bora 2020,kanda ya mashariki maonesho haya yameshirikisha washirika wa taasisi za umma na sekta binafsi ili kutoa elimu na kufanya wakulima ,wafugaji na wajasiriamali kujifunza mbinu mbali mbali na teknolojia mpya za kuendeleza shughuli zao za kiuchumi

Hata hivyoameongeza kuwa jumla ya washiriki 526 wamejiandikisha kushiriki katika maonesho haya ukilinganisha na washiriki 512 kwa mwaka jana nab ado tunaendelea kuwapokea washiriki wengine kwakuwa maonesho hayo ndo kwanza yameanza

Aidha amemuomba mgheni rasmi kuwasaidia ili mwakani  maonesho ya nane nane kitaifa yafanyike kanda ya mashariki katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Maonesho ya sherehe za nane nane kwa mwaka 2020 imepambwa na kauli mbiu inayosema ,KWA MAENDELEO YA KILIMO ,MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA October 04, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 22, 2021
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI TARAFA YA VIGOI March 14, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 May 06, 2022
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Bonanza la Uhuru lafana Ulanga

    December 08, 2023
  • Kuelekea Siku ya 9 December Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Ulanga wafanya usafi katika Hospital ya Wilaya

    December 06, 2023
  • Angalia Zaidi

Video

Link Kuripoti shuleni
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Vipindi vya Radio Ulanga
  • Majukumu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA FFARS
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

    Anwani ya Posta: P.O. BOX 22

    Telephone: +2550232626340

    Simu: 0763845957

    Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.