Zaidi ya kaya 50 zimejiunga na mfuko wa bima ya afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa katika uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wa kaya kwa kaya uliofanyika katika kata ya Minepa wilayani Ulanga.
Hayo yalisemwa na Meneja (CHF) wilaya Bi Sigirinda Mdemu wakati wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji kaya kwa kaya kwa mwaka 2017 ambapo alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia asilimia 80 ambayo ni lengo lililokusudiwa.
Aidha katika uzinduzi huo pia walishiriki viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao kwa pamoja waliadhimia kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na maafisa waandikishaji katika maeneo yao.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walihoji juu ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya vya serikali ikiwemo zahanati na hospitali za wilaya na kuongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakatisha tamaa ya kujiunga na huduma hiyo.
Akitoa ufafanuzi Dkt. Nataria Mtolela ambaye ni dakatri mshauri wa mradi humo ameeleza kuwa kwa sasa dawa aina nyingi zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya tofauti na zamani sababu maboresho mengi yamefanyika kuhakikisha madawa yanapatikana kwa wanachama wote
Vilevile Dkt. Mtolela alitoa wito kwa wananchi kujiunga na bima hiyo ili kupunguza gharama za matibabu na kwasasa wananchama wote waliojiunga watapata huduma katika mkoa wa Dodoma, Morogoro na Shinyanga tofauti na awali ambapo mwanachama alikuwa akihudumiwa sehemu aliyojiunga tu.
Chf iliyoboreshwa imezindua kampeni ya uandikishaji wa wanachama wapya kwa kupita kaya kwa kaya ili kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na wanapata huduma bora za afya kwa gharama ya Tshs. 10,000 kwa mwaka mzima kwa wanafamilia sita.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.