Na. Michael Lyachema
Mkuu wa wilaya ya ulanga Mh Ngolo Malenya amefunga mafunzo ya jeshi la akiba ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika tarafa ya rupilo
Akifunga mafunzo hayo Mh Malenya amewapongeza wakufunzi wa mafunzo na wale wote walioshiriki mafunzo hayo na hatimaye kumaliza mafunzo hayo kwani ilikuwa ni safari ndefu mpaka kuhitimu mafunzo hayo
Mh ngolo amesema kuwa ana imani kuwa mafunzo hayo yamewajengea ukakamavu ujasiri na kujiamini kwani kwa sasa wahitimu watakuwa tofauti na wasiofanya mafunzo hayo
“Nina imani ndugu zangu mafunzo haya yatasaidia sana kwenye ukakamvu kwani mtakuwa ni tofauti kabisa na wasio fanya mafunzo ya mgambo kwani kwa sasa mtakuwa na hali ya kujiaminina kuwa wajasiri kutokana n mafunzo mliyopata”
Aidha ameongeza kuwa wahitimu hao wanatakiwa kujua ulinzi wa nchi ni wa wananchi wenyewe hivyo kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza ulinzi wa nchi na kujilinda wao na familia zao
Kwa upande wa mshauri wa mgambo wilayani ulanga kevin byabato amesema kuwa mafunzo hayo yalianza 01.oktoba 2019 ikiwa na jumla ya wanafunzi 83na ilipungua hadi kufikia 57 waliohitimu kwani wengine walishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na utoro na magonjwa mbali mbali
“Mheshiwa mgeni rasmi wanafunzi hawa walianza wakiwa 83 lakini kutokana na sababu mbalimbali wengine waliacha kutokana na sababu kama vile utoro,afya na kushindwa kumaliza mafunzo na hvyo kufanya wanaohitimu kuwa ni wanafunzi 57alisema byabato”
mwisho

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Anwani ya Posta: P.O. BOX 22
Telephone: +2550232626340
Simu: 0763845957
Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz
Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.