• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Eneo la Utawala
    • Majukumu ya Viongozi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi na Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Radio Ulanga FM
      • Ijue Radio Ulanga FM
      • Vipindi vya Radio Ulanga FM

MH.Kebwe amewataka wakandarasi wanaojenga miundo mbinu kukamilisha kwa wakati

Imetumwa: September 8th, 2018

NA FATUMA MTEMAGA

Ujenzi wa miundo mbinu ya barabara ya kiwango cha lami na daraja la Mzingizi lililopo kata ya Sali wilayani Ulanga Mkoani Morogoro unatarajia kukamilika tarehe ishirini na tano mwezi wa kumi mwaka 2018 ili wananchi wa kijiji cha Isyaga waweze kupata huduma za msingi kwani huduma hizo zilisimama kutoka kana na miundo mbinu hiyo ya daraja kusombwa na maji wakati wa mvua za masika za mwezi wanne mwaka huu.

Akizungumzia ukamilishwa wa ujenzi huo mkuu wa mkoa wa Morogoro ndugu Kebwe Steven Kebwe amewataka wakandarasi wanaojenga miundo mbinu hiyo kukamilisha kwa wakati ifikapo tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka 2018 kwani hali ya hewa kwa Wilaya ya Ulanga sio ya kuridhisha  hii ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Hata hivyo dk.Kebwe aliwataka wakazi wa Sali kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayana itikadi ya chama hivyo wasiingize mambo ya siasa kwenye maendeleo ili kumuunga mkono mh.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dk.John Pombe Magufuli anavyosimamia shughuli za maendeleo bila kuangalia itika ya chama wala ukabila.

“Maendeleo hayana itikadi ya chama kila mtu anataka maendeleo kwani Zahanati si tunatumia wte,barabara,maji na shule tunatumia wote sasa wakandarasi nimeongea na nyie mmenielewa sasa nataka ufanye kazi kwa haraka mkamilishe ujenzi huu, leo una bahati sana na kama mkienda tofauti nawachukulia hatua  na kwa mkoa wa Morogoro tusingewapa tena kazi”.Alisema Kebwe

Pia mkuu wa mkoa amewataka wakandarasi hao wa kampuni ya Luqma Construction Com.Ltd na Mmeto Construction Com.Ltd kuwalipa vibarua kwa bei  elekezi ya viwango vya serikali ambapo kutwa moja ni wanalipwa shilingi elfu saba badala ya shilingi elfu kumi na tatu ambayo ni viwango vya serikali hivyo ametoa siku 5 kuandaa gharama walizo kuwa wanalipa vibarua hapo awali na ukamilishaji wa ujenzi huo na kuwasilisha ofisi ya mkuu wa mkoa saa mbili kamili asubuhi.

“Nataka nikija hapa tarehe ishirini na tano nikute barabara hii imeisha na daraja likamilike na sio kufanya uzembe halafu mvua zianze kunyesha iharibu tena na kuhusu hawa vijana wetu nataka muwalipe kwa makubaliano ya viwango vya bei elekezi ya serikali na kuwalipa kiholela holela tu haiko hivyo nataka barabara hii iishe sitaki uzembe na watu wa Tanroads nataka mfanye haraka kufanyia vipimo sampuli zinazoletwa ofisini kwenu.

Aidha mkuu wa nkoa amewataka wakazi wa kijiji cha Isyaga na Sali kutunza miundombinu ili huduma za msingi ziendelee ili iweze kupitika wakati wa mvua za masika na kiangazi kwani wapo watu wanapoteza maisha ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo kama miundo mbinu hiyo haitatunzwa serikali haitaleta fursa zingine katika maeneno hayo.

Ndugu zangu wakazi Sali na Isyaga mfanye kazi hii kwa vizuri kabisa na uaminifu kwa bidii kama ninavyowaona muwe na uzalendo ili barabara hii ikamilike hakuna kujiachia mimi katika ziara yangu nikija naongea na wafanyakazi mimi sitakuja kuongea na viongozi mkuu wa wilaya au mkurugenzi hata huko nilikotoka sikuongea na wakurugenzi wala wakuu wa wilaya hapana mmepata bahati ya kupata serikali inawajali sasa sitaki mfanye uzembe nataka nikija tarehe ishirini na tani barabara hii iiishe.

katika ziara yake mkuu wa mkoa amekagua miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Morogoro inayotekelezwa na ilani ya chama cha Mapinduzi {CCM} ambapo mradi wa barabara kilometa nane unatakiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na daraja la mto mzingizi lijengwe kwa umakini kutokana na daraja hilo kusombwa na maji mwezi wa nne wakati wa mvua za masika.

Mradi wa barabara ulianza kutekelezwa mwaka 2015/2016 kwa mkataba wa shilingi milioni mia nane thelathini na nne laki nne sitini na mbili elfu mia mbili na sabini na tano{834,462,275.60} unaotekelezwa na kampuni ya Mmeto Construction Com ambapo mradi huu ulisimama kwa mwaka mzima baada ya daraja linalounganisha sehemu mradi ulipo kusombwa na mafuriko lakini kwa sasa mkandarasi amekamilisha kuimarisha tabaka la juu kwa kuchanganya kifusi na saruji hivyo kazi zilizobaki ni kuweka matabaka ya lami na kujenga mifereji na ifikapo mwezi wa kumi mradi huo utakamilika.

 Ziara ya mkuu wa mkoa wa Morogoro dk. Kebwe Steven Kebwe katika wilaya ya Ulanga imekamilika kwa kugakua miradi ya maendeleo katika kata ya Ruaha kijiji cha Sali,Iyaga kwa kugagua ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa nane pamoja na daraja la Mzingizi ili kutekeleza ilani ya chma cha Mapinduzi .

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA October 04, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 22, 2021
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI TARAFA YA VIGOI March 14, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 May 06, 2022
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Bonanza la Uhuru lafana Ulanga

    December 08, 2023
  • Kuelekea Siku ya 9 December Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Ulanga wafanya usafi katika Hospital ya Wilaya

    December 06, 2023
  • Angalia Zaidi

Video

Link Kuripoti shuleni
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Vipindi vya Radio Ulanga
  • Majukumu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA FFARS
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

    Anwani ya Posta: P.O. BOX 22

    Telephone: +2550232626340

    Simu: 0763845957

    Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.