• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Eneo la Utawala
    • Majukumu ya Viongozi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi na Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Radio Ulanga FM
      • Ijue Radio Ulanga FM
      • Vipindi vya Radio Ulanga FM

halmashauri ya wilaya ya Ulanga yaadhimisha kilele cha upandaji miti kitaifa kwa kupanda zaidi ya miti mia moja na hamsini

Imetumwa: April 1st, 2019

Na Yuster Sengo

Ikiwa leo ni siku ya kilele cha upandaji miti kitaifa, wilaya ya Ulanga imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda miche ya miti zaidi ya 300 katika kijiji cha mbagula wilayani hapa

Akizungumza katika maadhimisho hayo ,Afisa tawala Bi Huruka Rajab ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ulanga Mh.Ngollo Malenya, amewataka wakazi wa kijiji cha Mbagula kitongoji cha ukwama kulinda na kuitunza miti hiyo ili ilete faida kwa vizazi vya sasa n avya baadae

Aidha ameongeza kuwa katika utunzaji wa mazingira ,tunaweza tukaboresha viwanda vyetu kwakuwa viwanda vya mbao au miti vinakazi nyingi sana ambapo tunategemea kupata vitu mbali mbali kutoka katika miti

“Tuitunze miti hii tunayoipanda leo kwakuwa inaweza kutuletea faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbao,karatasi,vibiriti,thamani za ndani kutoka viwandani ,hivyo ni jukumu la kila mtu kutunza mazingira na kutunza miti yetu”,Amesema bi Huruka

Aidha ameongeza kuwa miti imekuwa ni chanzo kizuri cha mvua na hali ya hewa nzuri lakini pia inasaidia katika majanga mbali mbali kama vile mafuriko na ukame hivyo hatuna budi kuitunza ili pia kuweza kufikia lengo la Halmashauri ya wilaya ya Ulanga ya kuwa na miti milioni moja na laki tano kila mwaka.

“Hivyo niwasisitize wanambagula,viongozi na mwenyekiti pamoja na serikali yako ya kijiji mtunze miti inayopandwa leo kwasababu kila mmoja wenu hapo anajua umuhimu wa miti na kutunza mazingira ,na ndiyo maana siku zote tunakumbushwa kuwa tutunze mazingira ili nayo yatutunze”Ameongeza Hurka

Naye mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Bw. Mohamed Atiki  ambaye alikuwa anamuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kila kaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua elfu 20 ili kufikia lengo la kiwilaya hivyo kuwataka wakazi wa ukwama kuilinda miti hiyo ili iweze kuleta tija hapo baadae

Hata hivyo mkuu wa idara ya mazingira Bw. Justine Bundu,amesema kuwa katika kilele cha upandaji miti kitaifa ,wilaya ya Ulanga imepanda miti  zaidi ya 150, wakati kiwilaya tunatakiwa kupanda miti milioni moja na laki tano na kwa mujibu wa idadi ya vijiji tulivynavyo wanatakiwa kupanda miti elf 20 kwa kila kijiji

Aidha ameongeza kuwa idara yake imeshaanza kupokea takwimu tangu zoezi lianze mpaka sasa hivi miti iliyopandwa ni zaidi ya miti  laki nne,na kwa miaka miwili ya nyuma tumeweza kupanda miti kwa asilimia tisini kwa 2016/2017 na mwaka 2018/2019 tumepanda kwa asilima 89 na kwa mujibu wa takwimu tulizokusanya ,asilimia zaidi ya sabiniimepona.

Hata hivyo tunategemea jukumu kubwa lausimamizi wa miti hii ni kutoka kwa viongozi wa kitongoji cha ukwama pamoja na wananchi kiujumla kuisimamia kwa ukaribu zaidi

“kuna changamato za usimamizi wa miti inayopandwa na ndiyo maana kwa sasa mikakati ya wilaya ni kupanda kwenye taasisi, maana miaka ya nyuma tulikua tunapanda sehemu za wazi lakini tukiondoka tu miche hiyo inaliwa na mbuzi na inaharibika lakini kwa kupanda kwenye taasisi tunaimani wahusika wataitunza vizuri “amesema Bundu

Maadhimisho ya siku ya kilele cha upandaji miti kitaifa,imeongozwa na kauli mbiu isemayo “TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA ,PANDA MITI KWA MAENDELEO YA VIWANDA

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA October 04, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI November 22, 2021
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI TARAFA YA VIGOI March 14, 2022
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 May 06, 2022
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Hakimu mfawidhi Ulanga atambulisha wiki ya sheria

    January 17, 2024
  • Bonanza la Uhuru lafana Ulanga

    December 08, 2023
  • Kuelekea Siku ya 9 December Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Ulanga wafanya usafi katika Hospital ya Wilaya

    December 06, 2023
  • Angalia Zaidi

Video

Link Kuripoti shuleni
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Vipindi vya Radio Ulanga
  • Majukumu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA FFARS
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

    Anwani ya Posta: P.O. BOX 22

    Telephone: +2550232626340

    Simu: 0763845957

    Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.