• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Eneo la Utawala
    • Majukumu ya Viongozi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi na Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Radio Ulanga FM
      • Ijue Radio Ulanga FM
      • Vipindi vya Radio Ulanga FM

Mkuu wa wilaya ya Ulanga awataka watumishi wote kufanya kazi kwa weledi

Imetumwa: September 27th, 2018

Na Fatuma Mtemangani

Mkuu wa wilaya ya ulanga Bi Ngollo Malenya amewataka watumishi wote waliopo katika idara mbalimbali kufanya kazi kwa weledi  kwa kutoa huduma kwa jamii na kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayopelekea kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya.

Bi. Ngollo ameyasema hayo wakati alipokutana na watumishi wote wilayani hapa katika ukumbi wa halmasahauri wa Pauline kuzungumza nao na kukemea vikali suala la majungu miongoni mwa wafanyakazi kwani hata livumilia katika uongozi wake hivyo upole wake usiwe kigezo cha kutotoa maamuzi kwa mtumishi.

Aidha ametoa wito kwa watumishi kuzingatia muda wa kuingia kazini na kutoka kazini pamoja na kufuata sheria ya mavazi ya kiutumishi kwani serikali haitamvumilia mtumishi atakae kiuka sheria na taratibu za kiutumishi.

“Upole wangu usiwe kigezo cha kunichukulia poa siku zote mtu mpole ana kitu ndani yake naomba tusicheze na kazi mimi ni Mchamungu sana ndiyo mana sipendi majungu na sipendi mtu aje ofisini kwangu kwa ajili ya kumsemea majungu mfanyakazi mwenzake hapana sijaumbwa hivyo na sitakuwa hivyo nichokitaka uje ofisini kwangu tushirikiane kufanya kazi na ndiyo maana Mh. Rais ameniteuwa kwakuwa ameniamini na nyinyi mfanye kazi kwa weledi na kushirikiana  ili tulete maendeleo wilayani hapa. ”.alisema Ngollo Malenya

Hata hivyo mkuu wa wilaya ameahidi kutoa ushirikiano katika idara ya elimu kwa kwa shule za msingi na sekondari kwa kuwahimiza wazazi na walezi kujitolea kufyatua matofali kwa kila kijiji kuwa na benki ya tofali ili zisaidie katika ujenzi wa vyumba vya madarasa,matundu ya vyoo,maabara pamoja na nyumba za walimu ambapo imekuwa ni changamoto kubwa kwa kila halmashauri nchini.

Pia ameanza ziara yake ya kuzunguka kila kijiji wilayani Ulanga kwa ajili ya kuzungumza na wenyeviti wa vijiji hivyo amewataka wasiwe maafisa ardhi kwa kugawa ardhi bila mpangilio na badala yake wafuate sheria na taratibu zilizowekwa za ugawaji wa ardhi ambapo kiwango chake ni hekali hamsini.

 Aidha ameongeza kwa kulitaka jeshi lapolisi wilayani ulanga kuchukua maamuzi ya haraka kwa kutenda haki kwa raia na mali zao pale wanapopeleleza kesi ili kusiwe na mrundikano wa kesi mahakamani na mahabusu gerezani  kwa kufuata sheri za utumishi wa uma.

Mwisho.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA 2018 December 10, 2018
  • Matokeo kidato cha nne January 24, 2019
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA ULANGA October 25, 2018
  • MALI ZINAZOKODISHWA NA HALMASHAURI YA WILAYA March 22, 2018
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • Kamati ya bunge ya Maliasili,Utalii na Ardhi yafanya ziara wilaya ya Ulanga,Kilombero na Malinyi

    February 06, 2019
  • baraza la madiwani lapitisha bajetiya zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa kipindi chamwaka 2019/2020

    January 31, 2019
  • mkuu wa wilaya ya Ulanga awataka madiwani kuwazuia wananchi wanao vamia maeneo ya hifadhi

    January 31, 2019
  • halmashauri ya wilaya ya ulanga imeshika nafasi ya pili kimkoa katika matokeo ya kidato cha nne 2018

    January 25, 2019
  • Angalia Zaidi

Video

Uzinduzi wa Daraja la Magufuli
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Vipindi vya Radio Ulanga
  • Majukumu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa
  • MFUMO WA PLANREP
  • MFUMO WA FFARS
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

    Anwani ya Posta: P.O. BOX 22

    Telephone: +2550232626340

    Simu: 0763845957

    Barua pepe: ded@ulangadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2017 Ulanga District Council . All rights reserved.